Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
0 comments:
POST A COMMENT