Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.
Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.
Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.
Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku.
Manji amefika kituoni hapo akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza. Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.
Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan.
0 comments:
POST A COMMENT