Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Oxford umeonyesha kuwa, asilimia 5 - 10 ya watoto wanaoambukikizwa VVU(HIV) wakati wa kuzaliwa huwa hawapati ugonjwa wa UKIMWI kutokana na aina ya kinga waliyonayo inayodhibiti virusi hivyo na kuzuia ugonjwa.
Asilimia 50 ya watoto wenye HIV hupoteza maisha kabla ya kufikisha miaka miwili, lakini watoto hawa wenye kinga madhubuti huishi maisha ya kawaida bila kudhania kuwa wana VVU.Habari hii ni kwa wa chuo kikuu cha Oxford, na ugunduzi huu ulichapishwa katika jarida la kitabibu la Science Transilational Medicine.
Huwa kuna idadi ndogo ya watu wazima ambao huambukizwa VVU lakini hawapati UKIMWI, na watafiti wamejaribu kufuatilia kwa miaka mingi ni kwa jinsi gani katika kujaribu kupata dawa. Lakini ugunduzi huu mpya umeonyesha kuwa, kingamwili za watoto hawa zinafanya kazi kwa jinsi tofauti ukilinganisha na watu wazima.Wataalam hao wanasema kuwa, ugunduzi huu unaleta tumaini jipya la kupatikana kwa tiba kwa wanaoishi na VVU.
Utafiti huo ulifanyika huko kusini mwa Sudan,na watafiti wamegundua ufanano wa ufanyaji kazi wa kinga za mwili za watoto hao na nyani wenye uambukizi wa SIV(virusi vinavyofanana na HIV). Nyani hao huwa hawapati ugonjwa japokuwa wanakuwa na idadi kubwa SIV katika miili yao.
Wanasayansi hao wanasema, utafiti zaidi unahitajika ili kuweza kufahamu kwa kinagaubaga ni kwa jinsi gani kinga ya watoto hao inavyoweza kupambana na VVU na kutoa mwanga zaidi wa jinsi ya kuweza kupambana na maradhi ya UKIMWI, na pengine kupata tiba ya uhakika.
0 comments:
POST A COMMENT