Mara nyingi ndoa huvunjika kutokana na tatizo la upunguvu wa nguvu za kiume. Dalili kuu za tatizo hili ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zilizo na uwezo wa kutungisha mimba. Pia, kutosimama kwa uume wakati wa kujamiiiana ni dalili nyngine ya tatizo hili.
Tatizo hili limewaathiri watu wengi kati mabara totafauti ulimwengu mzima. Takwimu zilizopo zinadhihirisha kwamba asilimia sitini ya wanandoa katika nchi tofauti tofauti wanakambiliwa na upunguvu wa nguvu za kiume.
Pia karibu ndoa 2 kati ya 5 zilizo na umri wa miaka miwili na kuendelea zinakambiliana na tatizo la kutoweza kumudu vizuri tendo la ndoa.
Jambo la kushangaza ni kwamba, ndoa nyingi amabazo zimevunjika kutokana na tatizo hili kwa sababu wahusika hawakuwajibika ipaswavyo ili kusuluisha tatizo hili. Badala ya wanandoa kufichuliana ukweli kuhusu tatizo hili, mara nyingi wanaume huficha kabisa na kuanza kumlaumu mwanamke kwa kukosa mtoto.
Wanaume wengi wameshauriwa kuwa kutumia madawa ya kuchochea nguvu wakati wa tendo la ndoa kunaweza kuwa suluhu. Nataka uelewe ya kwamba madawa haya yana madhara si haba.
Natumahi umesikia habari kuhusu wananume waliohaga kutokana na shida za moyo wakiwa vyumbani na vimanda wao. Kwa hivyo ongopa hayo madawa na pia uelewe kuwa ukitaka tiba stahiki la tatizo la upunguvu wa nguvu za kiume lipatikane, lazima kiini chake kichunguzwe kwa makini.
Nini kinachisababisha upunguvu wa nguvu za kiume?
Tatizo la nguvu za kiume huhusishwa na kuvaa ngua za kubana sana, kuugua kwa muda murefu, miozi ya compyuta au simu, ugonjwa wa kisukari, na mengineyo.
Pia, upunguvu wa nguvu za kiume husabibabishwa na kupiga punyeto kwa muda mrefu, matatizo ya kisaikolojia, dawa za wadudu ambo zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, na kutumia vyakula vilivyo na kemikali kwa muda mrefu.
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
watafiti wa masuala ya usihano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula hivi ni:
1. Pweza na chaza
Hizi ni aina za samaki ambazo huvuliwa baharini. Kulingana na watafiti, samaki hawa huwa na madini ya zinc na chumvi kwa wingi.
Madini hayo yanajulikana kwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinanvyoleta msisimko wa mwili wakati mume na mke wanajamihiana.
2. parachichi
Hili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E. Vitamini E husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume.
Kulingana na watafiti tofauti, watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali haswa wakati wa kufanya mapenzi. Pia, faida za tunda hili haziengemei upande wa wanaume pekee.
Katika upande wa wanawake, tunda hili husaidia kuongeza majimaji yaliyo na utelezi katika sehemu za siri za mwanamke ili kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa tendo la ndoa.
3. Karanga
Utafiti umebaini kuwa karanga ni chanzo kikuu cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia mwili kuwa na mfumo wa damu unaotakikana.
Ni vizuri kuelewa kuwa mwanamume huhitaji kiwango fulani cha mfumo wa damu ili kushiriki tendo la ndoa kikamilifu. Kwa hivyo, kiungo kikuu cha karanga ambacho ni amino asidi husaidia mwili kuwa na mfumo mzuri wa damu, hivyo, husababisha kiwango cha juu cha ufanyaji mapenzi.
4. kitunguu saumu
Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.
Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilishapolysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.
Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kinaallicin, kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.
Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.
5. Ndizi
Unapofikiria kufyanya vyema katika tendo la ndoa, unatakiwa kuwaza kuhusu uimara wa misuli ya mwili ambayo hutajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye umuhimu mkubwa katika kujamihiana.
Kwa msingi huo, hulaji wa ndizi mbivu husaidia kujenga misuli mwilini na pia kumfanya manamume kuwa hodari katika tendo la ndoa.
6. Chokoleti
Chokoleti huwa na viamabato kama vile alkaloid naphenylethylamine. Hivi viambato huongeza stamina ya kufanya mapenzi. Phenylethylaminehusaidia mtu kuhisi vizuri wakati wa kufanya mapenzi.
Kwa hivyo, kama una tatizo la kutoshiriki tendo la ndoa vizuri, jaribu kula chokoleti kila siku.
7. tikiti maji
Tikiti maji ni tunda ambalo lina faida nyingi sana katima mwili. Kwanza, tunda hili ni huwa na virutubisho kama vile potasium, calcium, magnesium, carotene. Pia, tunda hili huwa na vitamini muhimu sana kwa miili yetu.
Vitamini hizi ni kama vile vitamini A, B6, na C. Kwa hivyo, tikiti maji, haswa mbegu zake huupa mwili chembechembe muhimu za kuongeza kuvu za kiume mwilini.
8. mbegu za matunda
Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda kama ile maboga, tikiti, na matunda mengineo husaidia kupunguza asidi mwilini na kumfanya mtu awe na afya njema.
Ni vizuri kujua kuwa kuwa na afya njema husaidia mwanamume kushiriki tendo la ndoa ipaswavyo.
9. Mfinyo mwekundu
Utafiti umedhihirisha kuwa mvinyo mwekundu una wezo wa kuongeza msukumo wa damu. Elewa kwamba kiwango cha msukumo wa damu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa uume umesimama wakwati wa kujamiiana.
Pia, mfinyo mwekundu huuchangamsha mwili kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya kufanya mapenzi.
10. Tangawizi
Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Kwa hivyo, ni bayana kuwa kiungo cha mwanamume kinachoshiriki tendo la ndoa kitakuwa na damu ya kutosha na pia kusimama kwa muda mrefu. Pia, ulaji wa tangawizi husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
Kilele cha juu zaidi cha furaha katika ndoa yoyte ile, kama inavyojulikana, ni furaha inayopatikana wakati wa kufanya mapenzi. Ni vizuri kuelewa kuwa kuishiwa na nguvu za kiume kunaweza kuhusishwa na kuongezeka kwa umri.
Tafiti mbalimbali zinadhihirisha kuwa wanume wa umri kuanzia miaka 61 na kuendelea hupatwa na tatizo hili zaidi kulikuko wanaume wa miaka 41 kushuka chini.
Ni muhimu kuelewa kuwa kuna visababishi vya upunguvu wa nguvu za kiume ni vyingi.
Kwa hvyo, badala ya kutapata hapa na pale ukitafuta msaada au kugobana na bibi yako kila siku, jaribu vyakula amabvyo vimejadiliwa katika makala haya na utasaidika.
0 comments:
POST A COMMENT