Msanii wa filamu Aunt Ezekiel amefunguka kwa kudai kuwa ameshawahi kutoa mimba kadhaa lakini hajui ni ngapi
Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Cookie, akijibu swali la shabiki wake kupitia Kikaango cha EATV aliyetaka kujua idadi ya mimba ambazo amewahi kutoa, Aunty alisema hawezi kusema uongo kuwa hajawahi kutoa mimba, lakini kitu ambacho hakumbuki ni idadi ya mimba alizowahi kutoa.
“Kutoa nishawahi, nikisema sijawahi nitakuwa muongo, ila kukumbuka ni mimba ngapi ndiyo tatizo,”alisema staa huyo wa filamu.
Muigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano na dansa wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo, amesema kwa sasa anatamani zaidi kupata mtoto wa kiume atakamuita jina la Greyson ambalo ni jina la babu yake.
0 comments:
POST A COMMENT