DAR ES SALAAM Skendo ya mjini iliyotapakaa mjini na kwenye mitandao ya kijamii inamgusa modo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto akidaiwa kujichora ‘tatuu’ ya mwanamuziki maarufu Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, ishu iliyosababisha mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumporomoshea matusi.
Kuhusu sakata hilo, mama mzazi wa Mobeto ameshindwa kujizuia na kujikuta akimtolea povu Zari juu ya mwanaye huyo. Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu alipoulizwa kuhusu sekeseke hilo la mwanaye, mama Mobeto alisema kuwa, hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.
“Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema mama Mobeto. Alifunguka kuwa, habari ambayo imesambaa kuhusu mwanaye kujichora tatuu ya Diamond, anaona ni mambo ambayo hayana msingi wowote zaidi ya kumchafua na kumdhalilisha mwanaye.
“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya, kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” alisema mama Mobeto.
Hivi karibuni Zari alimtolea matusi Mobeto kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akimtahadharisha juu ya habari zilizozagaa kuwa, huwa anachepuka na Diamond kwa siri hasa mwanamama huyo anapokuwa nyumbani kwake, Afrika Kusini na kumwacha baba watoto wake huyo jijini Dar.
0 comments:
POST A COMMENT