Rais wa marekani Donald Trump amesisitiza msimamo wake kwamba alidukuliwa na utawala wa rais Obama ,akimwambia mgeni wake kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwamba kuna ''kitu kinachowaleta pamoja''.
Vikosi vya ujasusi nchini Marekani chini ya utawala wa rais Obama vilidaiwa kuipeleleza simu ya Angel Merkel hatua iliozua hisia kali.
Lakini viongozi wa Republican pamoja na wale wa Democrat wanasema kuwa hawaamini kwamba rais Trump alipelelezwa.
Bwana Trump na Bi Merkel wamejadiliana kuhusu Nato na biashara.
Ziara yake ilikuwa imepangiwa kufanyika Jumanne iliopita lakini ikaahirishwa kutokana na dhoruba ya theluji.
Bwana Trump alitoa madai yake ya kudukuliwa katika mkutano wa pamoja na bi Merkel.
Pia aliulizwa kuhusu tamko lake la katibu wa ikulu Sean Spicer kwamba GCHQ ya Uingereza ilimpeleke wakati wa kampeni za uchaguzi.
0 comments:
POST A COMMENT