MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetoa hati ya kukamatwa Msanii Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange (28), baada ya kushindwa kufika mahakamani mara kwa mara ya pili kesi yake ilipopangwa kutajwa.
Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Wilbroad Mashauri ametoa amri hiyo baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini mshtakiwa, wadhamini na wakili wa utetezi wote hawakuwepo mahakamani.
Wakili wa Serikali Adolf Nkini alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa lakini kwa sababu mshtakiwa na wadhamini wake hawakuwepo mahakamani kwa mara ya pili, aliomba hati ya kukamatwa mshtakiwa.
Hakimu alisema kwa sababu mara mbili mfululizo mshtakiwa ameshindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake bila taarifa mahakama yake inatoa hati ya kukamatwa kwake.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
0 comments:
POST A COMMENT