Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amedai wanaomuita shujaa leo ipo siku wanaweza kumgeuka kwa sababu kama binadamu bado ana safari ndefu na anaweza kujikwaa ndiyo maana hataki kulivaa jina hilo bali anahitaji watanzania waendelee kumuombea.
Akizugumza akiwa Mtama Mh. Nnauye amesema hawezi livaa jina hilo bali amelipokea kwakuwa wananchi wameamua kumpatia jina hilo kwani hata sababu za kuitwa jina hilo zipo tofauti tofauti.
"Sikatai kuitwa Shujaa kwa sababu wao wenyewe ndiyo wameniita, lakini siyo jambo ambalo nitalivaa. Hao hao wanaoniita shujaa siku nyingine wanaweza kunigeuka kwa sababu binadamu ukiwa hai unaweza kujikwaa safari bado ni ndefu nachotaka kuwaomba tu wananchi waendelee kuniombea. Hata hivyo sababu za kuitwa shujaa kila mtu ana sababu yake, mwingine atakuambia kwa sababu hujatetereka wengine wanasema umesimamia ukweli, kwa hiyo jina hilo siwezi kulivaa ila siwezi kulikataa". Alisema Nape.
Mh. Nnauye jana alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Mtama kwa mara ya kwanza baada ya kuvuliwa uwaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Machi 22 mwaka huu.
0 comments:
POST A COMMENT