MKAZI wa kijiji cha Kabita wilayani Busega mkoani Simiyu, Hezroni Mahila (28) amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma nyumba na kusababisha hasara ya Sh. 6,000,000.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa Simiyu, John Nkwabi, baada ya mtuhumiwa kukubali kutenda kosa hilo.
Awali kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Moses Mfuru, alieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Februari 24, mwaka jana, saa 8:00 usiku kwa kuchoma nyumba mali ya Kapeji Sostenes.
Baada ya kusomewa shtaka lake, mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa hakuisumbua mahakama lakini hakimu alimhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha.
0 comments:
POST A COMMENT