YAWEZEKANA kukawepo maneno mengi ya kuzungumza juu ya ukaribu wa wanamuziki wawili Emmanuel Simwenga ‘Izzo Buzness’ na mwanadada anayefahamika zaidi kwa jina la Abela Music, lakini kubwa ni juu ya kuhusishwa kwa wawili hawa kuzama kwenye dimbwi la mahaba. Tetesi juu ya mkali huyu wa michano Bongo kutoka na Abela zilianza kusambaa muda mfupi tu baada ya yeye kumdaka mwanadada huyo kutoka Ughaibuni alikokuwa anaishi kwa ajili ya masomo na kuunda kundi wakijiita The Amaizing.
BUZNESS AKANA UHUSIANO
Hata hivyo tetesi hizo za kutoka na Abela, ‘mzee baba’ Buzness amezikanusha mara kadhaa. Muda mwingine amekuwa mkali na kudai watu wanashadadia kitu ambacho si kweli. Kwamba yeye na Abela wapo kwa ajili ya kazi tu na baada ya hapo kila mmoja wao ana maisha yake mengine, jambo ambalo linapingana na vitendo pamoja na mienendo yao.
VITENDO VYAWAUMBUA
Mbali na Buzness kukanusha kutoka na Abela vitendo vinawaumbua. Ukweli ni kwamba wawili hawa ni kama kumbikumbi. Muda mwingi wanakuwa pamoja.
Katika kazi na sehemu tofautitofauti wakila bata na wanaowafahamu zaidi wanasema hata anapoishi Buzness mitaa ya Sinza B, mwanadada huyo anaonekana mara kwa mara jambo ambalo linazidi kuzua maswali zaidi. Acha na hayo, hivi karibuni Buzness na mwanadada huyo walikuwa kwenye shoo ya mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Fid Q pale kwenye Ukumbi wa Next Door, Masaki Dar. Wakiwa pale walionekana kuwa karibu mno.
Lakini kilichowafanya watu wapigie mstari tetesi juu ya wawili hao ni namna Izzo alivyokuwa anamkumbatia na hata alivyopanda jukwaani alipokaribishwa kuwasalimia mashabiki. Buzness alimpandishi mwanadada huyo pia jukwaani na kumtambulisha kuonyesha mahaba ‘live’ akimkumbatia na kuwauliza mashabiki walikuwa wanawaonaje.
MAPENZI YAWAZIDI NGUVU
Kutokana na hali halisi hivi ndivyo unaweza kusema. Inawezekana kabisa Buzness anajaribu kuficha juu ya uhusiano wake na Abela kwa masilahi fulani.
Lakini ukweli ni kwamba mapenzi yamewazidi nguvu na kama walivyosema Waswahili mapenzi ni kama kikohozi huwezi kuficha, limekuwa ni suala gumu kwa mkali huyo kuendelea kuwapiga kamba watu kuwa habanjuki kimalavidavi na Abela
MAKALA: BONIPHACE/GPL
0 comments:
POST A COMMENT