Aliyekuwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira akiwa katika jengo la Mahakama ya Rufaa jijiji Dares Salaam akizungumza jambo na baadhi ya mawakili kabla ya kusikiliza kwa Rufaa ya kesi yake dhidi ya Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya. Katika kesi hiyo jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa limepanga kuendelea na kesi hiyo Jumatatu ijayo ya Aprili 15, mwaka huu. Uamuzi huo umetolewa leo Aprili 11, mwaka huu katika Mahakama hiyo baada ya Pande zote mbili kutoa maelezo ya sababu za rufaa.
Wakili wa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Tundu Lissu akizungumza jambo na mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.
Wakili Constantine Mutalemwa akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari mara baada kikao kilichokuwa kinasikiliza ombi la rufaa lilifunguliwa na wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda, kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kuhusu ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya.
0 comments:
POST A COMMENT