Wednesday, 31 August 2016
UBONGO WA MTU UNA SELI 100 BILLIONI ZA MAWASILIANO
New Official Video: RAYMOND (RAYVANNY) NATAFUTA KIKI
BREAKING NEWS :MWENYEKITI WACHADEMA MBOWE HAAIRISHA MAANDAMANO YA UKUTA
Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es SalaamMuungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani, akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari Dar es Salaam.Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.Viongozi wa chama hicho walikuwa wameitisha maandamano na mikutano ya kisiasa Septemba Mosi kupinga walichosema kuwa ni ukandamizaji unaoendelezwa na serikali.Baada ya mkutano wa kikao cha Kamati Kuu ya chama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwishoni mwa Julai, viongozi walisema: "Yapo Matukio ambayo yamekua yakifanywa na kukandamiza demokrasia na misingi ikipuuzwa na kudharauliwa."
Viongozi wa upinzani Tanzania kuhojiwa zaidi
Maafisa wa Chadema wakamatwa Tanzania"Si nia ya Chadema kugombana na Serikali bali ni kazi ya Chama Pinzani kuisaidia Serikali iongoze kwa kufuata misingi ya Katiba," chama hicho kilisema.Maandamano hayo yalipewa jina Ukuta, ikisimamia Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania.
=Bw Lowassa, ambaye aliwania urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka 2015
Serikali ilipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa, ya hadhara na ya ukumbini. Baadhi ya viongozi wa upinzani wamekamatwa na kuzuiliwa kwa muda.
CHANZO BBC SWAHILI
Weka Picha za Utupu Mtandaoni Uende Miaka 20 jela – TCRA
Tuesday, 30 August 2016
Lipumba: Mimi bado ni Mwenyekiti wa CUF, sitambui kikao cha Zanzibar
Hii safi sana maana maalim anaendesha chama kama mali yake.
Akihojiwa na mtangazaji Spencer Lamerk wa ITV usiku huu, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF.
Prof. Lipumba amesema kuwa kufuatia kutengua barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti, aliandika barua kwa Katibu Mkuu wake kutaka kurejea kazini kama Mwenyekiti. Katibu Mkuu alimjibu kuwa anatafuta ushauri wa kisheria.
Kuhusu kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomsimamisha uanachama, Profesa Lipumba amesema kuwa kikao hicho hakikuwa halali kwakuwa hakukuwa na akidi ya Wajumbe wa kutoka Tanzania Bara. Amesema kuwa Katibu Mkuu hamshirikishi Naibu Katibu Mkuu Bara na kuonekana akiendesha chama kiimla.
Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu asipotaja tarehe ya yeye kurejea kazini kama Mwenyekiti, atasubiri barua ya Msajili wa Vyama ili aanze kazi tena kama Mwenyekiti wa taifa wa CUF.
Maghembe apiga marufuku usafirishaji mbao usiku
SERIKALI KUTOA AJIRA MPYA 71, 496 HIVI KARIBUNI
UVCCM WASALIMU AMRI ... WAAHIRISHA MAANDAMANO YAO
Waziri Mkuu Akaribisha Wawekezaji Kutoka Japan.
Lipumba Aendelea Kung'ang'ania Uenyekiti Wake CUF
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.
“Kikao hicho hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba
Lipumba aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho.
“Nilimuandikia barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba.
Aidha aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini mkutano ule ukavurugwa.
Kuhusu kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa mara nyingi huwa hamuAelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kifuata misingi ya kidemokrasia.
“Katibu Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu Bara, mara nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu sasa anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze wanachama, wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza, hizo ni dalili za uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali demokrasia na siyo kuwa dikteta ndani ya chama” Amesema
Kuhusu Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba amesema kuwa hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama kiongozi wa chama hicho bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye ndiye aliyempa.
“Mtatiro hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama, Mtatiro alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”
Taarifa Kwa Umma Kuaribika Kwa Mashine ya MRI Hospitali ya Taifa Muhimbili
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inapenda kuujulisha umma kwamba mashine ya MRI itasimama kwa muda kufanya kazi baada ya kuharibiika. Mashine hii iliharibiika tarehe 24/08/2016 baada ya kutokea hitilafu ya umeme.
Baada ya kuharibiika, tarehe hiyo (24/08/2016) mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wetu walianza kutafuta athari baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.
Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi.
Hospitali ya Taifa Muhimbili inawaomba radhi wananchi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa na;
John Stephen, Ofisa Uhusiano,
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Mchezaji Mpira Avunjiwa Mkataba Baada ya Kugundulika Ana Virusi vya Ukimwi
Zikiwa zimepita siku nne tu tangu asajiliwe na klabu ya Al Ittihad inayoshiki ligi kuu ya Misri, Samuel Nlend, 21, mkataba wake umevunjwa baada ya klabu yake mpya kugundua mchezaji huyo anamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Jarid linalojulikana kwa jina la KingFut.com limeripoti kuwa, afisa habari wa klabu hiyo amethibitisha taarifa hiyo ya kusikitisha kwa vyombo vya habari.
Mshambuliaji huyo ameitumikia Cameroon katika michezo mitano, alifunga goli January kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kabla ya kujiunga na Al Ittihad majira ya kiangazi.
Samuel Nlend alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Al Ittihad tangu tarehe 24 August. Licha ya hayo yote kutokea bado amepata support ya kutosha kutoka kwa klabu yake mpya ya Misri.
Waliochuma watumishi hewa matatani
SERIKALI imeanza kuwashughulikia watumishi walionufaika na fedha za watumishi hewa ambapo hadi sasa watumishi 839 wapo katika hatua mbalimbali wakiwemo waliofikishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na wengine wanaendelea kuhojiwa polisi kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Sambamba na hilo, serikali inatarajia kutoa ajira mpya 71,496 kwa mwaka huu wa fedha baada ya kukamilisha uondoaji wa wafanyakazi hewa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki aliyasema hayo wakati akizungumzia utekelezaji wa mipango na mikakati ya wizara yake katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Kairuki alisema,
“Kwa sasa tayari wapo watumishi wameshahojiwa na kuchukuliwa maelezo yao polisi na upelelezi utakapokamilika watachukuliwa hatua mbalimbali za kisheria, ikiwemo kufikishwa mahakamani… Tunakamilisha ushahidi na tutawatangazia tutakapokamilisha,” alisema.
Alisema waligundua kwamba kuna maofisa utumishi na wahasibu ambao siyo waaminifu, badala yake walikuwa wakielekeza fedha kwa ndugu zao na miradi yao na wengine walishastaafu lakini bado majina yao yalikuwa yakiendelea kupokea mishahara wakati walitakiwa kuondolewa kwenye mfumo.
Alisema kwa kipindi cha Machi mosi hadi Agosti 20 mwaka huu, watumishi hewa waliogundulika ni zaidi ya 16,127 na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha. Kwa kipindi cha Agosti pekee watumishi hao hewa wangelipwa mishahara wangeisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 16.
“Uhakiki huu ni endelevu na tumegundua changamoto kubwa katika usimamizi wa mishahara ni uadilifu kwa watu waliokasimiwa madaraka. Maofisa Utumishi, Maofisa Utawala na Wahasibu wamepewa madaraka lakini wengi wao siyo waaminifu, hivyo kwa sasa tumeweka uwajibikaji kwa waajiri,” alisema.
Aidha alisema wanaufanyia mfumo wao maboresho zaidi ili uweze kuchakata taarifa nyingi zaidi ambapo pia sekta ya mishahara imeshushwa katika ngazi za chini zaidi hasa katika sekta za elimu na afya ambazo zimekutwa na watumishi hewa wengi zaidi ili waweze kuwa na taarifa za mtumishi mmoja mmoja.
Alisema upo muongozo ambao fedha za serikali zinaporejeshwa zinapitia hazina na kusisitiza kwamba wataendelea kuhakikisha wanasimamia fedha zote ambazo zilichukuliwa serikalini kinyume na utaratibu na isivyo halali zinarudishwa kwa mfumo sahihi.
Pia alisema wameongeza kasi ili kuhakikisha kunakuwa na nidhamu ya kazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo wanaanda mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma na ikiwezekana utaanza kutumika mwaka ujao wa fedha.
Alisema serikali imefanya maboresho makubwa katika mishahara na motisha kwa ajili ya maslahi ya watumishi wa umma, sambamba na kuhimiza taasisi mbalimbali kuweka vitendea kazi ili kuwawezesha wafanyakazi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumzia ajira hizo mpya Kairuki aliwatoa hofu watanzania waliokuwa wanatarajia ajira serikalini na kusisitiza kwamba walichokuwa wanasubiri ni takwimu halisi kwa taasisi ili kujua ni watumishi wangapi wameondolewa.
“Baada ya kukamilisha mchakato huo, hatua nyingine zitaendelea… Hii ni neema kwa waliomaliza vyuo, cha msingi wavute subira maana tutatoa ajira 71,496 kwa mwaka huu wa fedha na hatukuzifuta ajira. Nawashauri vijana wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa wasubiri ajira zinakuja,” alisema. Katika hatua nyingine, Kairuki alisema, wamepokea malalamiko zaidi ya 200 kutokana na ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa Utumishi wa Umma ambayo inamnyima mtumishi kutotumia madaraka yake vibaya.
“Katika malalamiko hayo 142 yanahusu sheria ya maadili. Sekretarieti ya Maadili imefanya uchunguzi wa awali na malalamiko 12 yataanza kufikishwa Baraza la Maadili na hatua mbalimbali zinaweza kuchukuliwa ikiwemo kushushwa vyeo au kuachishwa kazi,” alisema.
Pia aliwaagiza maofisa utumishi kuwahudumia watumishi na kuwapa haki zao ikiwemo kuwapandisha madaraja kwa wakati pale wanapostahili. Aidha Kairuki alikemea tabia ya baadhi ya watu kughushi taarifa za utumishi wa umma na kusisitiza kwamba jambo hilo ni kosa kubwa kwa yeyote anayefanya hivyo.
“Mtu yeyote ambaye anatoa nyaraka za serikali na siyo mlengwa au anayetoa nyaraka ambayo imewekewa zuio kwa mujibu wa sheria ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Tunawasisitiza watumishi wa umma kuhakikisha wanazingatia sheria hizo na mwongozo wa utoaji nyaraka na kumbukumbu za taarifa za serikali,” alisema.