Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amewataka wafanyabiashara waliopewa vibali vya kuvuna na kuuza bidhaa za misitu hususani mbao, kusafirisha mizigo yao nyakati za mchana ili kuepuka udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiasha.
Profesa Maghembe ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano baina yake na wadau wa masuala ya misitu, mkutano ambao pamoja na mambo mengine ulikuwa unajadili uvunaji holela wa rasilimali za misitu.
Kwa mujibu wa Waziri Maghembe, tabia ya kusafirisha mbao nyakati za usiku imekuwa ni moja ya njia inayotumiwa katika ukwepaji wa ushuru pamoja na uvushaji wa mbao zilizovunwa kwenye aina ya miti ambayo haistahili kuvunwa.
0 comments:
POST A COMMENT