AFA BAADA YA BUNDUKI YAKE KUJIFYATUA WAKATI AKIWINDA | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 8 September 2016

AFA BAADA YA BUNDUKI YAKE KUJIFYATUA WAKATI AKIWINDA

Baba wa watoto wawili amefariki dunia baada ya kujipiga risasi mwenyewe kwa bahati mbaya wakiwa katika safari usiku kuwinda sungura akiwa na rafiki yake.Carl Rubisch, mwenye miaka 30, alifariki kwa kujeruhiwa na risasi moja alipokuwa akitembea kuelekea lango la shamba wakati wa mawindo hayo yaliyopangwa karibu na Brockton mjini Shropshire.Rafiki wa Rubisch alikimbilia kwenye nyumba za jirani na kumwambia mmiliki apige simu kuita gari la wagonjwa lakini madaktari hao hawakufanikiwa kumnusuru na akafariki dunia kwenye eneo la tukio Ijumaa usiku.Mkewe Fay, mwenye miaka 29, alikuwa amechanganyikiwa mno kiasi cha kushindwa kuzungumza jana kwenye nyumba yao ya shambani humo huko Lichfield, Staffordshire.Majirani walisema wanandoa hao walifunga ndoa chini ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita na walifanikiwa kupata watoto wawili.Fay, ambaye aliolewa na Rubisch Juni mwaka jana, alielezewa kuwa asiyetulizika baada ya kumpoteza 'rafiki yake kipenzi na mwenzake wa karibu'.Mkazi mmoja, ambaye hakupenda kutaja jina lake, alisema: "Carl alipenda uwindaji wake wa bunduki - kama alivyo baba yake ambaye ni mwanachama wa Klabu ya British Falconers."Sikuweza kuamini pale niliposikia kilichotokea. Ni makini mno hivyo sipati picha walivyopoteana."Nimemwona Fay na anaonekana asiyetulizika kabisa. Amempoteza rafiki yake mkubwa na mtu wake wa karibu - walifunga ndoa mwaka uliopita tu.
"Walikuwa wakitarajia kufurahia maisha yao yote pamoja. Hakika hili ni janga kubwa."Marafiki pia wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamiiMpelelezi Inspekta Mark Bellamy, kutoka Polisi wa West Mercia, alisema: "Inaonekana bunduki yake mwenyewe muathirika ilifyatuka na kumjeruhi vibaya.""Polisi wanaendelea kuchunguza mazingira ya tukio zima lakini wamesema inaonekana kuwa ni ajali ya kawaida."

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us