Kila kukicha vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya inazidi kupamba moto, wakati mataifa mbalimbali yakizidi kuimarisha udhibiti wa biashara hiyo, na wafanyabiashara hiyo wanazidi kuja na mbinu mpya za kusafirisha dawa hizo.
Huko Colombia mwanamke mmoja raia wa Canada amekamatwa uwanja wa ndege akiwa na tumbo la ujauzito wa bandia ambalo ndani yake alificha kilo mbili za dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Polisi wa uwanja wa ndege wa Bogota Colombia alimshtukia mwanamke huyo raia wa canada Tabitha Leah Ritchie aliyeonekana kuwa na tumbo lisilo la kawaida ndipo baada ya kumkagua wakakutana na dawa hizo.
0 comments:
POST A COMMENT