Kwenye kitabu kimoja nilichowahi kusoma, kuna habari ya jeshi lilokwenda vitani. Baada ya wanajeshi wote kuvuka daraja kuwaelekea maadui jemedari mkuu akaamua kuchoma moto lile daraja, magari na kila kitu ambacho kingewawezesha kukimbia ikiwa vita ingewaelemea.
Kisha akawageukia wanajeshi wake akawaambia, "Chagueni kushinda vita ama kufa kwa sababu kukimbia ama kurudi nyuma haiwezekani tena". Jeshi lile lilishinda vita! Mbinu hii nimepata kuitumia nilipofanya rasmi maamuzi ya kujiajiri pindi nilipomaliza chuo kikuu.
Nilijua kwenye kujiajiri kuna changamoto nyingi na kuna hatari nikakata tamaa na kutafuta ajira. Nikaamua kuchoma madaraja yote yanayoweza kunifanya nikimbie kujiajiri kwenda kuajiriwa! Kwanza kwa makusudi sikuchukua cheti cha matokeo wala cheti chochote wala barua inayothibitisha nimemaliza chuo kikuu; pili nilijiapiza kutoshughulika na matangazo, habari ama taarifa zozote kuhusu ajira. Nikabaki na option moja tu ya kuhakikisha napambana kufa na kupona kwenye kujiajiri mpaka kieleweke.
Haikuwa kazi rahisi, lakini sikuwa na namna zaidi ya kutoka ama kufa. Nilikataa kufa na leo ninasonga mbele kwa mafanikio. Ninachokuhakikishia ni kuwa ukiamua kwa moyo mmoja kufanikiwa katika jambo lolote; ni lazima utafanikiwa, no matter what!! Kama stori nzima haijakuvutia, chukua sentensi moja ya mwisho!
By SmartMind
0 comments:
POST A COMMENT