Dar es Salaam. Jakaya Kikwete na Edward Lowassa walikuwa marafiki na sasa ni maadui wakubwa wa kisiasa, lakini jana walilazimika kushikana mikono wakati wa ibada ya kuaga mwili wa kada wa CCM, Didas Masaburi.
Mbali na tukio hilo, Rais John Magufuli alituliza wafiwa alipoeleza kuwa Masaburi, ambaye alizikwa jana chuoni kwake Chanika Dar es Salaam, ameacha wake wapatao watano na watoto zaidi ya 20 baada ya minong’ono kuibuka kutokana na aliyesoma wasifu kusema kada huyo ameacha mke mmoja wa ndoa na wajane wawili.
0 comments:
POST A COMMENT