Aliyekuwa mwanamuziki mashuhuri duniani, Lucky Dube wakati wa uhai wake
Siku kama ya leo, Oktoba 18 mwaka 2007, mwanamuziki mashuhuri duniani, Lucky Dube alifariki dunia. Katika kumbukizi ya kifo hicho, Waziri wa Sanaa na Utamaduni, Natji Mthethwa amewataka raia wa Afrika Kusini kumkumbuka mwanamuziki huyo kwa kumuombea.
“Leo tunatoa heshima zetu kwa mwanamuziki huyu, muziki wake uliwaguza mamilioni ya watu duniani,” amesema
Mthethewa aliendelea na kumpongeza Dube akisema kuwa muziki wake ulianza tangu kipindi cha Apartheid.
Dube aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la Rosettenville, Johannesburg.
0 comments:
POST A COMMENT