Mambo hayakuwa mazuri kwa watanzania baada ya kutofanikiwa kupata tuzo hata moja kwa wasanii wote ambao walikuwa wakiliwakilisha taifa katika tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA).
Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii kutoka Tanzania ambao walikuwa wakiwania tuzo hizo na alikuwa na haya ya kuwaambia mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya utoaji wa tuzo hizo kumalizika.
“Shukran sana sana kwa kura na sapoti kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa… pia S/O tu my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kamwe tusisononeke.. kuingia tu watanzania wengi kwenye MtvAwards ni hatua kwa Muziki wenu na ushinndi tosha kwa taifa letu…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award…my hommie @jahprayzah and @wizkidayo ya’all deserve the Trophies….”
0 comments:
POST A COMMENT