Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 1 October 2016

Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus

Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus

ImageNdege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 244

Shirika la ndege la Rwanda, Rwandair, limezidisha ushindani katika uchukuzi wa ndege Afrika Mashariki na Kati kwa kununua ndege aina ya Airbus A300-200.

Ndege hiyo itawezesha shirika hilo kufika masoko ya Ulaya na bara Asia.

Ndege hiyo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa kimataifa wa Kanombe, Kigali.

Tanzania yanunua ndege zake mbiliNdege ndefu zaidi duniani yapata ajali

Mkuu wa shirika la Rwandair John Mirenge amewaambia waandishi wa habari kuwa ndege hiyo yenye nafasi ya abiria 244 ndiyo ya kwanza katika ukanda huu na ina teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu.

"Ukiwa angani ndani ya ndege hii unaweza kupiga simu, kupata ujumbe wako wa simu, ujumbe wa barua pepe, ujumbe wa WhatsApp na mawasiliano mengine. Haya hayakuwepo katika ndege nyingine tulizo nazo," amesema.

"Hata katika ukanda huu na kwingineko barani afrika hakuna shirika lenye ndege iliyo na uwezo huo."

Ni ndege iliyotengenezwa nchini Ufaransa na kununuliwa kwa kitita cha dolla milioni 200 za marekani.

ImageSafari ya kwanza ya ndege hiyo itakuwa kwenda Dubai

Bw Mirenge, anasema safari za shirika la ndege la Rwandair zilikuwa zinajikita sana Afrika magharibi na kati na kwamba ndege hii sasa inakuja kuongeza uwezo wa kuvamia masoko ya Ulaya, Asia na kusini mwa Afrika.

Safari ya kwanza ya ndege hiyo inatarajiwa kufanyika wikendi ijayo tarehe 8 kuelekea mjini Dubai.

Shirika hilo sasa linalenga kusafirisha abiria laki 750 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.



google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us