Gari aina ya Nissan x-trial ambalo namba zake za usajiri hazikuonekana kwa haraka likiwa limeanza kushika moto upambe wa mbele na kupelekea kuteketea gari lote. tukio hilo limetokea jioni hii kando ya barabara ya Nyerere na usoni kabisa mwa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii, Jijini Dar es salaam, huku baadhi ya wasamalia wakijaribu kuokoa sehemu ya vitu vilivyokuwemo ndani ya gari hilo. hakuna alepoteza maisha wala kujerugiwa katika ajali hii. Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika. Picha na Zainab Nyamka.
Moto ukiendelea kuwaka kwa kasi.
Harakati ya kuokoa baadhi ya mali ziliyokuwepo ndani ya gari hilo zikiendelea.
Baada ya muda moto ukaenea sehemu kubwa ya gari hilo, hali iliyopelekea waokoaji kushindwa kuendelea na zoezi hilo.
Moto ukiiteketeza gari hiyo.
0 comments:
POST A COMMENT