Jumuiya ya wanafunzi taasisi ya Elimu ya Juu,(Tahliso), imesema imebaini kuwa baadhi ya wanafunzi hawakuwasilisha vyeti vinavyohakiki hali zao ikiwamo vyeti vya vifo vya wazazi huku baadhi wakishindwa kuvithibitisha kwa kamishna wa viapo.
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugaliza katika taarifa ya Jumuiya hiyo iliyotolewa baada ya kufanyIka kwa kikao cha dharura kilichoshirikisha Wizara ya Elimu na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu wiki iliyopita.
Kadugalize amesema walibaini makosa hayo baada ya kuwataka wanafunzi hao waliokosa mikopo kuwasilisha majina yao.
Amesema kasoro nyingine zilizofanywa na wanafunzi hao ni kutumia namba ya mtihani tofauti na ile aliyoitumia katika udahili wa chuo Tume ya Vyuo Vikuu nchini.
Taarifa hiyo ya Tahliso iliwataka wanafunzi hao kukata rufaa sasa kwa sababu dirisha lipo wazi na ni bure.
0 comments:
POST A COMMENT