Kozi mpya ya Washington University huko St. Louis, Marekani, itakuwa ikiangaza ulimwengu wa Kanye West.
Imeripotiwa kuwa, wanafunzi 75 wamejiandikisha kusoma kozi hiyo iitwayo, “Politics of Kanye West: Black Genius and Sonic Aesthetics” ambayo imeanza kufundishwa wiki hii.
Profesa Jeffrey McCune wa chuo hicho, anasema kozi hiyo imejikita katika maisha ta rapper na producer huyo na inalenga kuwasaidia wanafunzi kuelewa masuala ya siasa, rangi, jinsia, mapenzi na utamaduni.
Hiyo sio kozi ya kwanza ya chuo kuhusu West. Chuo kikuu cha Georgia State nacho kilitoa mwaka 2015, na mwaka 2014 kulikuwa na kozi katika chuo kikuu cha Missouri kuhusu West na Jay Z.
0 comments:
POST A COMMENT