‘Scorpion’ mwingine aibuka Sinza DSM, anajiita Van Damme | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 19 January 2017

‘Scorpion’ mwingine aibuka Sinza DSM, anajiita Van Damme


Leo January 19 2017 kupitia Leo tena ya clouds FM Mtangazaji Geah Habib ametuletea hekaheka kutokea mitaa ya Sinza makaburini Dar es salaam.

Hekaheka hiyo ni kuhusu jamaa ambaye amekuwa akifanya matukio ya uhalifu ikiwemo kuchukua mali za watu kibabe kama vile simu, jamaa huyo anajiita ‘Van Damme’. Wananchi wa eneo hilo wamesimulia kuwa ‘Van Damme’ akifika maeneo hayo maduka yanafungwa na madereva bodaboda wanamkimbia……..

‘Amani hakuna huu mtaa yaani ikifika saa moja, yeye ni saa moja hadi saa nne mwisho anaondoka hata wale madereva bodaboda na tax wakimuona amefika wanamkimbia mpaka atakapoondoka ndio wanarudi’;-Mwananchi

‘Yupo Van Damme jina lake halisi Ayub nilisharipoti polisi nikawaelezea wakasema walimtoa kwa makubaliano kwamba akitoka asifanye matukio, tangu atoke hawajapata ripoti yoyote ya matukio na wao hawawezi kumkamata bila ya kuwa na ripoti yoyote’;–Mjumbe 

‘Serikali wanamjua vizuri kwa sababu kashafanya matukio huko nyuma tena makubwa makubwa na amekaa ndani muda mrefu nafikiri mwaka au miaka miwili katolewa ndio huyo yuko mtaani anajulikana, ni familia ambayo tunaijua na mzazi wake tulikuwa tunamfahamu, Serikali inamjua ila inataka watu waende wakaripoti‘;-Mjumbe


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us