Hii tena kali Unamkumbuka Yule Babu wa Loliondo?kaibuka na Haya Mapya Juu ya Ile Dawa Yake ya Kikombe | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 21 January 2017

Hii tena kali Unamkumbuka Yule Babu wa Loliondo?kaibuka na Haya Mapya Juu ya Ile Dawa Yake ya Kikombe


Unamkumbuka yule Babu wa Samunge au Loliondo? Jina lake halisi anaitwa Ambilikile Mwasapile. Babu huyo pia ni mchungaji.

Mchungaji Mwasapile bado yupo na shughuli zake za kutoa kikombe cha dawa anayodai inatibu magonjwa  yote yanayomkabili binadamu.

Hata hivyo, baada ya ukimya wa muda mrefu babu ameibuka na kuitaka kwa mara nyingine Serikali kuboresha miundombinu ya Loliondo kwa kuwa kuna mambo makubwa yanakuja kutokana na maono anayoonyeshwa. 

Akizungumza nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale jana, Mchungaji Mwasapile alisema watu waliokuwa wanakwenda kwa wingi miaka iliyopita wamepungua sana na sababu ni kuwa idadi kubwa ya walipokea uponyaji wakati huo.

Mchungaji huyo mstaafu alisema wito anaoutoa kwa Serikali kuboresha miundombinu unatokana na mambo makubwa anayoonyeshwa yatakayokuja wakati ambao Mungu ameupanga.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us