KINGAZI BLOG: February 2017

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday, 28 February 2017

CHEBENAKO a.k.a ( Midondoko Sokomoko) Song__WAUZA MADAWA


Hii ndiyo jamii ambayo Anayekamatwa kwa Uchawi, Huliwa Nyama Yake huko Guinea



WAKATI ulaji wa nyama za watu ukitajwa kuwa hufanywa kutokana na matambiko maalum ya baadhi ya makabila nchini Papua New Guinea, kuna wengine wanasema ulaji upo kwa ajili ya dawa.
Wapo wanaopinga kutokana na ukweli kwamba kuna wakati Wazungu saba waliliwa kwa mpigo kama tutakavyoona katika matoleo yajayo ya makala haya kiasi cha kusababisha serikali kushtuka na kuanza kuwasaka waliofanya kitendo hicho kibaya.
Hakika ulaji wa nyama za watu siyo kwa ajili ya matambiko. Wakorowai ambao ndiyo kabila linaloongoza kwa kula nyama za watu nchini humo, vijana wao wanaochaguliwa kuingia katika kazi ya kuua, kukatakata nyama za watu na kuzipika, kwanza huchanjwa chale nyingi mwilini kwa kitu chenye ncha kali kisha kupakwa dawa. Vidonda hivyo vikipona huacha alama  ambazo watafiti waliokwenda kulitembelea kabila hilo walizipa jina la tattoo japokuwa hizo ni chale. Wakati wa kuchanja chale hizo, kijana hufungwa kwa kamba mikononi ili asiwe na uwezo wa kumzuia mchanjaji wakati akifanya kazi zake.


Mara baada ya kuchanjwa, hupakwa dawa ya kienyeji ambayo huzuia damu kutoka japo inasababisha maumivu makali kwa mtu aliyechanjwa. Baadaye mtu aliyechanjwa hupelekwa kwenye Mto Ndeiram Kabur  ambao hutumika sana kwa kusafiri kutoka vijiji vya kabila hilo hadi sehemu nyingine ya nchi.
Watafiti Waingereza waliokwenda kwenye makazi ya kabila hilo la Korowai wanasema siku ya kwanza kwenda kwenye vijiji hivyo walikwenda kwa kutumia mtumbwi kupitia mto huo.
“Tulipofika sehemu fulani tulishitukia tukivamiwa na watu waliokuwa uchi, mtu aliyekuwa akitutafsiria, Bwana Kembaren alisema watu hao walikuwa wanashangazwa na ngozi yetu,” alisema mtafiti mmoja.
“Nilimuona mtu mmoja, pande la mtu likiweka sawa mshale na upinde yule mtu aliyekuwa akitusindikiza (guard) akasema tuache kupiga makasia, tukatii, mtumbwi ukawa unaserereka.
“Hatukuwa na ujanja, walitoa amri ya sisi kushuka kwenye mtumbwi, kwa kweli tuliogopa sana kwani tulijua sasa ni zamu yetu ya kufanywa kitoweo na watu hao,” alisema mmoja wa watafiti hao.
“Hatuna nia ya kuwadhuru,” alisema mmoja wa wale watu, mfasiri wetu Kembaren aliwaambia kwamba tulikwenda huko kwa amani, hatukuwa na nia mbaya. Mmoja wa wale watu wakiwa watupu aliwasogelea lakini mkalimani wao, Kembaren alisisitiza kwa Wazungu hao kwamba watulie na wasiwe wamepaniki kwani kufanya fujo yoyote kutasababisha kifo kwao.
Baadaye Wazungu wote wakawa kama mateka na walipelekwa katika moja ya kijiji na ikatolewa maiti ya chifu wao aliyekaushwa kwa moto anayejulikana kwa jina la Moctezuma ili dua maalum ifanyike, hawakuelezwa dua hiyo ilikuwa kwa ajili ya nini lakini ilielezwa ikiwa mtu anauawa ili kuliwa,  nyama ya sehemu ya paja iliyokolezwa pilipili huwekwa karibu na maiti hiyo kibandani.
Kitendo cha maiti hiyo kutolewa nje kiliwatisha watafiti hao kwani waliwahi kusikia simulizi hiyo, hivyo wakajawa na hofu na wengi wakawa wanatokwa jasho la uoga wa kuliwa. Baadaye ngoma ilipigwa na wenyeji walijaa kuwashuhudia Wazungu hao, kiongozi wao alitumia nafasi hiyo kuwahutubia wananchi wake. Hata hivyo, mwandishi Mwingereza aliyeandika habari hii alisema hakuwa anaelewa kile alichokuwa akisema kiongozi yule wa kimila.
Kabila la Korowei lipo nyuma sana kimaendeleo na limetajwa kwamba ndilo lililohusika kumpika supu kijana Michael, mtoto wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani, Nelson Rokeffeller  aliyepotea kiajabu na hakuonekana tena na baadaye kujulikana kwamba aliliwa.
Kabila hili lina taratibu moja, licha ya kula watu lakini kama mwanaume anakamatwa kwa kujihusisha na uchawi, adhabu yake naye huwa ni kuliwa nyama yake, kitendo hicho kwa lugha yao hukiita khakhua.

Monday, 27 February 2017

Wachawi wa Nchini Marekani Waapa Kumroga Donald Trump Atoke Madarakani


Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani.

Lakini wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo.

Usiku wa manane siku ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini.

Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500.

Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita vya kiroho.

Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika machi 26.

Chama cha wakiristo nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo.

Hata hivyo Trump hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.

Kamanda Sirro: Nasumbuliwa Sana na Wanawake Usiku

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa nyingi kwenye kazi yake.

Kamishna Sirro afichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.

Amesema kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.

"Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi". Amesema Kamanda Sirro

Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza  na mara nyingi huwa anachukua hatua.

Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa jeshi la polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa

Diamond Platnumz Apata Dili Jingine la Mamilioni

Mwanamuziki Diamond Platnumz amezidi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki barani Afrika na nje ya Afrika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wasanii wengi wakubwa wanaozidi kumuongezea mashabiki katika mataifa mbalimbali.

Hivi karibuni Diamond alipotoa video ya wimbo wa Marry You alimshirikisha mwanamuziki Ne-Yo kutoka nchini Marekani aliuweka katika akaunti yake mpya ya Youtube ambayo ipo chini VEVO.

Diamond ni miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye akauti ya VEVO ambapo wanalipwa kutokana na matangazo yanayowekwa wakati wa kutazama video na pia kulingana na idadi ya watazamaji.

Diamond Platnumz ameeleza kwanini alichelewa kujiunga na huduma VEVO na kwanini sasa hivi amejiunga nayo. Kupitia ukurasa wake ameandika;

Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia: “uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida….

SABABU YA KUYASEMA HAYA:
Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh…🙏 -SIMBA #MALENGO

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 27


Sunday, 26 February 2017

Taarifa Muhimu: TCU yatolea ufafanuzi uhakiki wa wanafunzi wasiokuwa na Sifa Vyuoni

Tume ya Vyuo  Vikuu  Tanzania (TCU)  inapenda kuuarifu umma kuwa, uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu

hufanyika kwa mujibu  wa Kifungu  5(1)(b)(c)  cha Sheria ya

Vyuo Vikuu Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.

 

Katika kutekeleza jukumu hili Tume ilianza zoezi la uhakiki kuanzia mwezi Agosti 2016. Hadi kufikia Februari 2017 zoezi

hilo lilikuwa limekamilika kwa vyuo 67 kati ya 84 vinavyotoa shahada ya kwanza. 

Hii ni mara ya kwanza uhakiki wa sifa za wanafunzi wa vyuo  vyote nchini kufanyika kwa wakati mmoja.  Lengo  la uhakiki lilikuwa kujiridhisha kuwa wanafunzi waliopo vyuoni ni wale waliodahiliwa kwa mujibu wa  sheria na taratibu  na kwamba wanakidhi vigezo  stahiki.

 

Uhakiki ulifanyika kwa kulinganisha taarifa za TCU na zile zilizowasilishwa na vyuo.  Uhakiki huo  ulihusisha jumla ya wanafunzi 131,994 waliopo vyuoni kwa mwaka wa masomo 2016/17.

 

Baada ya kulinganisha orodha zilizowasilishwa na vyuo na ile ya TCU ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8  wana sifa stahiki.  Aidha jumla ya wanafunzi 8,167 sawa na asilimia 6.2 tu walibainika kuwa na kasoro  katika taarifa za sifa zao.

Kufuatia hali hiyo, Tume ilitoa taarifa kwa umma kuwaomba wanafunzi kurekebisha dosari hizo  kwa kuthibitisha taarifa zao  kupitia vyuo  husika ifikapo  tarehe 28  Februari 2017  ili kuweka kumbukumbu sahihi za mwanafunzi.

 

Hata hivyo  imebainika kuwa taarifa hiyo  imepokelewa kwa mtazamo na hisia tofauti na hivyo kusababisha mkanganyiko vyuoni. Umma unaarifiwa kwamba haikuwa nia wala lengo la Tume kusababisha mkanganyiko huo.

 

Kwa kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya Tume na kutokana na maombi ya wadau  mbalimbali,  Tume sasa  itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo  katika kukamilisha zoezi hilo. 

Hivyo  wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu  na kuendelea na masomo  yao kama kawaida.

 

Aidha ifahamike kuwa wanafunzi waliokuwa wameorodheshwa siyo kwamba wamethibitika kuwa hawana sifa stahiki bali kuna dosari katika taarifa zao. Ndiyo sababu Tume iliwaomba kuthibitisha taarifa zao  ili kuondoa dosari hizo.

 

Imetolewa na

Kaimu Katibu Mtendaji

24 Februari 2017

Je, ulikuwa ukiyajua haya kabla??

UMEWAHI ONA HII...

💞chumvi ikizidi kwenye wali weka kiazi mviringo katikati kikiwa kimemenywa chumvi itapungua.

💞kama choo chako, kina harufu, ya mkojo na huna dawa washa kiberiti chooni harufu itakwisha

💞chukua ganda la limao lichome na vipisi vya karafuu weka kila pembe ya chumba mbu utawasikia kwa jirani

💞kutoa harufu kwenye wali uliongua weka kipande cha mkaa harufu ya kuungua itakata

💞km umepika mchuzi upo maji maji yaani mwepesi labda maji yamezidi chukua kiazi kikune na cha kukunia nyanya weka chuzi litakuwa rost

💞kuivisha maharage faster chukua maji yalochemka tia maharage weka kwenye chupa ya chai funga kesho mimina kwenye sufuria pika nusu saa harage litakuwa lishaiva

💞ukipika mchuzi vitunguu vikiungua weka sukari kidogo harufu ya kuungua haitasikika

💞Ukiamaliza kuosha vyombo still wire iweke kweny maji haiharibiki utaendelea kutumia kesho

💞big g ikiganda kwenye nguo weka kweny friza ikiganda itatoka kirahisi

💞kuondoa harufu ya uvundo kwenye fridge weka baking soda kwenye kikombe na maji kidogo weka kwenye fridge

Ukiipenda mpe au share na mwenzio

Mađãda poa Dar waanza kushughulikiwa

MKUU wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ali Hapi, ametoa onyo kwa wamiliki wa baa wanaowahifadhi watu wanaojihusisha na biashara ya ngono ‘Machangudoa’ kuwa watafutiwa leseni.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Kijitonyama waliodai kuwa kuna baadhi ya baa zimekuwa zikiwahifadhi wanaouza miili, hali ambayo ni hatari kwa mazingira na makuzi ya watoto.

Hapi amesema haiwezekani serikali iwe inapambana na biashara hiyo haramu lakini kuna baadhi ya baa zinawafuga machangudoa.

"Tutashughulika na changudoa na tutashughulika na wenye baa zinazowahifadhi machangudoa, kwa sababu hili ni suala lililo kinyume cha sheria, serikali inapambana na hili tatizo halafu mwingine analikumbatia, hilo haliwezekani, tutawachukulia hatua za kisheria," amesema.

Awali, akitoa malalamiko yake kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete, mkazi wa Kijitonyama alidai kuna baa zilizogeuka kero kwao.

Ameitaja baa iitwayo Kona ya Sinza imekuwa ikiwahifadhi machangudoa hivyo kuhatarisha makuzi ya watoto kwa kuwa wanaweza kuiga tabia zisizofaa.

"Hii baa iko hapo Afrika Sana, machangudoa wako pale wanajiuza hadharani, sasa kwa kweli hii ni kero kubwa kwetu, watoto wanaweza kuiga na matokeo yake tutakuwa na kizazi kibaya ," amesema mwananchi huyo.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA TAREHE 26 / 2 / 2017



































 

Gallery

Popular Posts

About Us