MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Rais Dk. John Magufuli atakuwa kiongozi wa kwanza nchini kuvunja rekodi ya kutawala kwa kipindi cha miaka mitano badala ya 10 kama walivyofanya watangulizi wake.
Mbowe aliyasema hayo jana wakati akizindua tawi la wakereketwa wa chama hicho lililopo eneo la Mpakani, Kata ya Kwakifua, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katika hoja hiyo, Mbowe alisema Rais Magufuli ataongoza kwa muhula mmoja kwa kuwa utawala wake hauthamini utu wa binadamu, na ikiwa vinginevyo, yuko tayari kuachana na siasa. “Watu wa Tanga mmechelewa sana kuiondoa CCM madarakani, tulifanya makosa kumchagua Rais wa Awamu ya Tano, matokeo yake wote tunaisoma namba. Tunaanza maandalizi mapema, maana huyu rais atatawala miaka mitano na akiendelea naacha siasa,” alisema Mbowe. #Mtanzania .
JE NI KWELI ANAYOSEMA MBOWE??? TUPIA COMMENT YAKO HAPA
0 comments:
POST A COMMENT