Aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba uteuzi wake umetenguliwa.
Hali hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuuzuia mkutano huo ambapo RPC Kinondoni alifunga barabara kwa gari kuzuia Gari ya Nape huku akiwataka waandishi wa habari watawanyike mara moja.
==> Haya ni machache ambayo Nape kayaongea
1.Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia.
2.Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola.
3.Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo.
4.Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.
5.Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka.
6.Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?
7.Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.
8.Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali.
9.Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.
10.Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza
11.Vijana naomba msimamie haki yenu
0 comments:
POST A COMMENT