Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amesema jeshi hilo linawasaka watu wanaofurahia mitandaoni na kukebehi baada ya askari wake kuuawa.
IGP ameyasema hayo wakati Miili ya Askari nane wa Jeshi la Polisi ikiagwa leo Mkoani Pwani.
IGP Mangu amesema, tulitumue tukio hili kama changamoto, ili tupeane nguvu badala ya kukatishana tamaa. Kuna watu wameanza kukejeli kwenye mitandao baada ya hili tukio kutokea, mheshimiwa Waziri nakuhakikishia tutawasaka hao wanaoendeleza kejeli badala ya kutupa pole wanakejeli na wengine wanafurahia.
Na mtu wa namna hii anefurahia si mwingine isipokuwa ni mhalifu kama huyu aliyefanya tukio hili baya, nao tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria tutakapowapata.
Ila tu niombe wananchi tutumie tukio hili kama changamoto na tutiane nguvu ili mwisho wa siku tuweze kushinda hii vita ya uhalifu kwa sababu hakuna mtu anayependa uhalifu na wote tunapenda amani.
0 comments:
POST A COMMENT