TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA WATANZANIA | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 20 May 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA WATANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WA WATANZANIA

RAISI WA SERIKALI YA WANAFUNZI ST. JOSEPH AFUKUZWA CHUO KWA KUTETEA HAKI ZA WANAFUNZI WENZAKE

Katika hali ya kusikitisha sana na yenye kuumiza moyo kijana Bachubila Haruna ambae ni Raisi wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Cha Mtakatifu Yosefu kampasi ya luguruni amejikuta akipoteza haki yake ya msingi ya kupata elimu katika taifa lake kwasababu ya kutete haki za wanafunzi wenzake.

Mnamo Tarehe 27/03/2017 Raisi Bachubila aliandika barua kwenda Wizara ya Elimu na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) akiomba mrejesho wa serikali kutokana na maagizo aliyoyatoa Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako (mb) kwa uongozi wa chuo na Tume ya Vyuo Vikuu kuhakikisha Elimu na Mazingira ya kusomea Chuoni hapo yanaridhisha wakati wa mgomo wa wanafunzi uliofanyika mapema mwaka jana 2015. Pia Raisi Bachubila alitoa malalamiko ya matatizo mbalimbali na kuomba msaada kutoka ngazi hizo za juu.

Baada ya kuandika Barua hiyo taarifa kupitia mawakala wa Chuo walioko TCU ziliwafikia wahindi ambao ndio wamiliki wa chuo hiko na kwa hali ya kushtukiza walimuandikia Raisi Bachubila barua wakimlaumu kwa kuwasiliana na wizara bila kuwapa taarifa wao, kukichafua chuo nje na kuandika taarifa za uongo.

Baada ya hapo ukapita mda kidogo na kilikuja kukaliwa kikao cha inquiry committee( kamati ya nidhamu ya chuo) kumjadili na kumhoji Raisi Bachubila mnamo tarehe 02/05/2017. Kikao hiko kikatoka na maazimo ya kuishauri seneti ya chuo kupitisha maamuzi ya kumsimamisha chuo mwaka mmoja Raisi Bachubila.

Wakati maamuzi ya seneti yanasubiriwa kukawa kunatokea vuta ni kuvute baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo wakitaka kujua nini hatma ya Raisi wao. Wakati huo huo Uongozi wa Chuo kipitia Dean of Students ukawa unamuita Raisi Bachubila ukimlazimisha aandike barua ya kukana barua alioandika kwenda wizarani na ajiuzulu nafasi yake.

Bachubila alikataa kufanya hivo na kubaki na msimamo wake wa kua mtetezi wa wanafunzi wenzake.

Kwa bahati nzuri sana tarehe 16/05/2017 Raisi Bachubila alipokea barua kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kupitia Katibu mkuu Wizara ya Elimu ikimjibu Raisi Bachubila kua imepokea na ikaipa maagizo Tume ya Vyuo Vikuu kufuatilia malalamiko hayo. Katika hali isiyo ya kawaida Raisi alishangazwa kupokea barua yake ikiwa tayari imeshafunguliwa na inaonyesha kucheleweshwa kupewa maana barua hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu iliijibu tarehe 08/05/2017.

Baada ya barua hiyo kuja siku iliyofuata tarehe 17/05/2017 Chuo kilimuandikia Rasmi Raisi Bachubila kua kimemfukuza chuo kupitia Principal wa chuo.

Wanafunzi wengi hatujafurahishwa na hatua hii na tunaipinga vikali. Kwani ni uonevu wa wazi kwa mtetezi wetu. Msimamo wake juu ya maslahi yetu ya Elimu ndio umesababisha leo hii amefukuzwa chuo. Hivo sisi kama wanafunzi tuko tayari kufanya lolote hata kama ni kuacha shughuli za kitaaluma mpaka pale mwenzetu, kaka yetu na kiongozi huyu atakapo rudishwa masomoni kwa nafasi yake ile ile ya Uraisi.

Mbali na hapo serikali iyopita ya wanafunzi ilikua ikiwasiliana na wizara na TCU hadi kufanikiwa kumleta Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako hapa chuoni ila hata siku moja haikuwahi kukipa chuo Taarifa yoyote na hamna kiongozi yoyote wa serikali zilizopita aliewahi kufukuzwa chuo kwasababu ya kudai haki katika mamlaka husika.

Ni ukweli kusema kwamba Chuo hiki cha St. Joseph ndugu watanzania wenzetu kimegubikwa na uchafu na wizi mkubwa wa kitaaluma na fedha za watanzania. Hapa chuoni tunalipa ada kubwa TSH 3000000/= na tunalazmishwa kuilipa yote kwa mkupuo lakini cha kushangaza katika idara mbalimbali wameajiri walimu wakihindi ambao hata elimu ya kuweza kufundisha Chuo Kikuu hawana ila tunalazmishiwa hivo hivo wakati hata lugha ya kufundishia ambayo ni kingereza hawajui.

Chuoni kwetu mitihani imekua ikisahishwa ovyo ili kuwapa wanafunzi Suplementary nyingi. Hatukatai kua hata katika vyuo vingine vya uhandisi Supp hutolewa kwa wingi ila tofauti ni kua wenzetu hao hua hawalipii Supp ila sisi tunalipia Supp shilingi 10000/= kwa somo moja. Hivo uongozi wa chuo umefanya kama mtaji wa kupata kipato cha ghafla.

Ikumbukwe kua Chuo hiki kilinyimwa intake ya wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza mwaka uliopita huku wizara ikikipa mda wa kujifanyia marekebisho ili kipate intake mwaka huu, ila cha kushangaza chuo kimeendelea na utaratibu mbovu usiokidhi.

Tunawaomba watanzania kwa ujumla, Viongozi wa nchi na Wizara pamoja na TCU waliangalie hili kwa jicho la tatu maana kama chuo hiki kitaendelea kutoa wahandisi feki basi ni hatari mno kwa maendekeo ya taifa letu.

Tunawaomba wadau mbalimbali wa Elimu nchini na wapenda haki kuingilia kati swala hili maana sisi wanafunzi na uongozi wa chuo inaonekana hatuwezi kufikia muafaka bora. Wanahabari mtusaidie kutangaza hili ili jamii ijue kiundani kinachoendelea St. Joseph.

Tchaooo
IMG-20170520-WA0013.jpg

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us