SHILOLE KIUNO -: VIDEO YA “NATAFUTA KIKI” ILIKUWA ZAIDI YA MTIHANI KWANGU. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 10 September 2016

SHILOLE KIUNO -: VIDEO YA “NATAFUTA KIKI” ILIKUWA ZAIDI YA MTIHANI KWANGU.

Toka mwaka huu uanze tumekwisha muona mwanadada Shilole kwenye videos za ngoma tofauti tofauti akishiriki kama video queen.
Baadhi ya ngoma hizo ni kama “Hainaga Ushemeji” ya Man Fongo, “Too Much” ya Darassa na hivi sasa tumemuona akitokea kwenye video ya “Natafuta Kiki” yakwake Raymond wa WCB.
Kwa upande wa mwanadada Shilole anasema kwamba video ya “Natafuta Kiki” ndio video ambayo ilikuwa ngumu sana kwake kutokana na kilichoimbwa humo ndani na yeye ilikuwa hana budi kuuvaa uhusika.
Na kwasababu anadai nia yake ilikuwa ni kutaka kumsaidia msanii mwenzake Raymond hakuwa na budi kufanya chochote kile kilichotakiwa kufanya japo kuwa mengine yalikuwa magumu na huenda yangemdhalilisha au kujivunjia heshima kwa mdogo ake Raymond lakini yeye wala hakulijali hilo.
Kwenye video hiyo tulimshuhudia mwanadada huyo akiwa kwenye Night Dress na akifanya mambo flani hivi ya kikubwa, kitu ambacho kilikuwa ni kigumu sana kwa mwanadada huyo kufanya na Raymondukizingatia alikuwa anamchukulia kama mdogo wake na vitu kama hivyo.
Ilimbidi mwanadada Shilole kunywa pombe kwanza ilikuweza kuchangamsha akili na kuweza kujiondoa aibu ili aweze kuuvaa uhusika kisawasawa.
“Ilikuwa mbaya sana kwangu, lakini nikaona maji ndo nimesha yavulia nguo kwahiyo sina budi kuyaoga. Ilikuwa ni ngumu sana lakini ilibidi ninywe pombe kidogo ili niweze kuchangamka. Nilivaa Night Dress, na script za scene ile zilikuwa haziruhusu kuvaa kitu chochote ndani, kwahiyo pale sikuvaa kitu chochote ndani, nilikuwa very naked.”
Ni maneno ambayo aliyazungumza Shilole alipokuwa akihojiwa na E-News ya EATV.


Unaweza kuitazama hapa video hiyo ya “Natafuta Kiki” ya Raymond (rayvanny) wa WCB.



google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us