Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ ambaye haishi vimbwanga, Alhamisi hii amefunguka kwa kudai kuwa hamjui msanii, Ruby ambaye aliwai kufanya vizuri na wimbo ‘Na Yule’
Aidha amedai pia hamjui video queen Giggy Money ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye video ya ‘Inde’.Akiongea katika kipindi cha Papaso cha TBC FM Alhamisi hii, Diva aliulizwa endapo akikutana na Ruby ambaye ameachana uongozi wake wa zamani atamshauri nini, ndipo mtangazaji huyo alipojibu kwamba hamjui msanii huyo.“How is Ruby? Simjui na sijawai kumsikia,” alisema Diva.
Hata hivyo, Diva hakueleza nini kilitokea kati yake na msanii huyo ambaye aliibuliwa na Serengeti Super Diva 2014 na baadae kupewa msaada zaidi na THT pamoja na Clouds FM.
Saturday, 10 September 2016
MTANGAZIJI DIVA WA CLOUDS FM ASEMA HAMJUI RUBY NA GIGY MONEY
Published Under
TOP STORIES
About Author
BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
POST A COMMENT