WATU 15 wamepoteza maisha nchini Bangladesh baada ya moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji katika kiwanda kimoja.
Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa kwenye tukio hilo lililotokea pembeni mwa Mji Mkuu wa nchi hiyo, Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga dunia ikaongezeka zaidi.
Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.
0 comments:
POST A COMMENT