KAMA kawa, kama dawa leo Mpaka Home imemleta kwenu mrembo anayefanya Muziki wa Hip Hop ambaye ni zao la Kundi la Navy Kenzo, Rosa Robert ‘Rosa Ree’.
Mrembo huyo anaishi Mapinga Wilaya ya Bagamoyo. Anaishi na dada yake na shemeji yake. Twende pamoja chini ili uweze kujua mengi zaidi kumhusu yeye anapokuwa nyumbani:
Ni kitu gani hapendi kukifanya na anachokipenda akiwa nyumbani?
“Napenda sana kupika lakini kuna kitu ambacho sikipendi japokuwa nakifanya kwa kuwa ni lazima nikifanye ni kuosha vyombo, bora nipike kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ni kitu gani kinachompa furaha na amani nyumbani?
“Napata sana amani na furaha nikiwa karibu na ndugu zangu kwa sababu wao wananipa sapoti kubwa ya kila kitu kwenye harakati zangu ni watu wanaonitia moyo sana wa kuzidi kusonga mbele na kufanya mambo yangu yaende sawa.
Mlo wake wa kila siku upoje?
“Unaweza kucheka, hivi sasa nipo kwenye diet na pia utashangaa kwa nini nafanya hivyo wakati sina mwili kabisa lakini hii ni sababu ya kutaka kufanya mwili wangu kuwa na afya bora siyo bora afya, hivyo nakula vitu vya kujenga mwili kama matunda na mboga za majani kwangu ndiyo mpango mzima.
Nini anapendelea kukifanya akiwa toilet?
“Huwa napenda kufanya mazoezi ya kuimba, nyimbo zangu nyingi natungia toilet. Ndiyo kuna utulivu mzuri. Ukiwa unaendelea na mambo, mistari inapanda kwelikweli. Ndiyo sehemu pekee ambayo naona kwangu inakuwa ya private zaidi ambayo naweza kufikiri mambo yangu na kuimba nyimbo ninazozifikiria.
Miaka 10 baadaye anafikiria kuwa nani?
“Nitakuwa mwanamuziki mkubwa sana siyo Tanzania pekee mpaka nje ya nchi na ninaamini ndoto hiyo itakamilika kabla hata ya hiyo miaka kwa sababu najikubali sana na nina amini ninachokifanya.
Anapenda wageni wa aina gani, anawaandalia nini?
“Sichagui mgeni mradi tu awe wa nia nzuri na pia ukiniambia unakuja kwangu sifikirii mara mbili najua chakula cha wengi ni pilau hicho ni kitu muhimu sana kwa wageni wangu na ninatumaini kila mtu anapenda chakula hicho.”
0 comments:
POST A COMMENT