Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kufuatia vifo vya watu kadhaa vilivyotokea kufuatia tetemeko la ardhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Katika salamu hizo Rais Dkt. Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake kufuatia tukio hilo ambapo idadi kubwa ya watu wamepoteza maisha wengi kujeruhiwa na uharibifu wa mali.
Rais Magufuli amesema anaungana na familia ambazo zimepoteza ndugu jamaa na marafiki na anawaombea kwa Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani, Amen.
‘Kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Mstaafu Mustafa Kijuu na wakuu wa Mikoa ya jirani yakoiliyokubwa na tukio hili natoa pole kwa familia ndugu jamaa na marafiki wote waliopoteza jamaa zao, nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu”Amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Dkt Magufuli amewaombea wote walioumia kufuatia tetemeko hilo wapone na kurejea katika hali yao ya kawaida na kuendelea na majukumu ya taifa.
Kwa taarifa ambazo zimethibitishwa kutoka mkoani Kagera watu 11 wamepoteza maisha na wengine 120 wamejeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera Augustine Olomi amethibitisha kutokea vifo hivyo na kusema zoezi la uokoaji linaendelea likihusisha taasisi ya Msalaba Mwekudu.
0 comments:
POST A COMMENT