Watu wawili wamenusurika kifo baada ya gari dogo aina ya taxi kuwagonga wananchi waliokuwa katika mazoezi asubuhi ya leo Jumamosi Machi 18,2017 mjini Iringa huku mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akinusurika.
Ajali hiyo imetokea nje ya lango la kamanda wa polisi mkoa dakika tatu tu baada ya kuanza mazoezi kuelekea uwanja wa Samora.
Ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na uzembe wa dereva aliyekaidi amri ya askari wa usalama barabarani ambao walisimamisha gari hilo lililokuwa likitoka mwelekeo mmoja na wafanya mazoezi hao.
Majeruhi hao wamepata michubuko kiasi mwilini huku mkuu wa mkoa ambaye alikuwa karibu na majeruhi huyo hakuumia na gari hilo japo alikuwa karibu na majeruhi hao .
Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa
Askari polisi wakiwa wamemkamata dereva taxi aliyesababisha ajali
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia akimtazama mmoja kati ya majeruhi waligongwa na gari asubuhi hui wakiwa katika mazoezi
SOURCE:KAMANDA WA MATUKIO BLOG
0 comments:
POST A COMMENT